Ulinzi mkali wakati wa Kesi ya Sheikh Issa Ponda; Farasi Mbwa watumika



Kiongozi wa Askari magereza, akiwaongoza Sheikh Ponda na wenzake, kutoka mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, baada ya kuahirishwa kwa kesi yao.
Sheikh Ponda Issa Ponda, akifunguliwa pingu, baada ya kufikishwa kwenye chumba cha mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana Alhamisi Novemba 1, 2012.

Askari wa kutuliza ghasia magereza, akiwa ameshika lindo mbele ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Alhamisi Novemba 1, 2012
Polisi wa Mbwa nao walichukua nafasi yao
Huiingii mahakama ya Kisutu bila ya kukaguliwa na mashine za kugundua vitu vya asili ya chuma hapo.
Farasi wa polisi wakiwafukuza wafuasi wachache wa Sheikh Ponda, waliojikusanya nje ya uzio wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Alhamisi Novemba 1, 2012
Polisi wa Mbwa wakisubiri amri ndani ya gari lao nje ya mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Novemba 1, 2012
Polisi wa Mbwa akifanya doria kwenye barabara ya Bitbi Titi mbele ya jengo la mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
Askari Magereza wa kutuliza ghasia, aliyejihami kwa silaha na vifaa vingine akiwa makini kulinda usalama

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB