MAKAMU WA RAIS DKT. BILLAL AWAISILI MKOANI KATAVI LEO NA KUZINDUA MIRADI MBALIMBALI PAMOJA NA TATHMINI YA KONGAMANO LA UWEKEZAJI LA UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya mara baada ya kushuka katika uwanja wa ndege wa Mpanda jana kwa ajili ya kuzindua Tathmini ya Kongamano la Uwekezaji la Ukanda wa Ziwa Tanganyika lililofanyika Wilayani Mpanda tarehe 17 Oktoba Mwaka 2011.


 
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akikagua vikundi vya ngoma katika uwanja wa ndege wa Katavi
 
Mama Zakhia Billal akiteta jambo na Mama Tunu Pinda katika jukwaa kuu kwenye uwanja wa ndege wa Katavi kabla ya uwanja huo kuzinduliwa jana na Makamu wa Rais.
 
 Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kukamilika kwa maborsho ya uwanja huo, kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba, kushoto ni Mama Zakia Bilal mke wa Makamu wa Rais.


 Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akizindua rasmi uwanja huo uliogharimu fedha za kitanzania shilingi bilioni 30 ambapo katika hizo bilioni 28 ikitolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na bilioni 2 zikitolewa na Shirikia la Kimataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akiteta jambo na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Chizeba katika uwanja wa ndege wa Katavi jana.

Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba akimkaribisha Makamu wa Rais ili kuongea na wananchi wakati wa uzinduzi wa uwanja huo mjini Mpanda jana.
 

 Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza wakati wa uzinduzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi jana mchana.
 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba muda mfupi kabla ya mapokezi ya Mkamu wa Rais jana Mjini Mpanda.

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Chadema Said Alfi katika uwanja wa ndege wa Mpanda muda mfupi kabla ya mapokezi ya Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Billal.

 Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mst. Issa Machibya wakijadiliana jambo jana katika katika mapokezi ya Makamu wa Rais katika uwanja wa ndege wa Mjini Mpanda.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Kimanta muda mfupi baada ya mapokezi ya Mhe. Makamu Rais katika uwanja wa ndege wa Mpanda jana.
 

 Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Mary Nagu akifurahia jambo na Mkuu wa  Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya katika mapokezi ya Mhe. Makamu wa Rais katika uwanja wa ndege wa Mpanda.
 
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe akizungumza katika kongamano hilo kwenye ukumbi wa Idara ya maji mjini Mpanda na kukaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria kongamano hilo.
 
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na kutoa taarifa ya mkoa wake wa Rukwa katika maendeleo ya uwekezaji.
 
Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Mary Nagu akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika mjini Mpanda jana.

Popular posts from this blog

TASWIRA: UZINDUZI RASMI WA KAMPENI ZA CHADEMA KWA UDIWANI WA KATA NNE ZA ARUSHA

RAIS KIKWETE ASAIDIA KUENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA WODI YA DHARURA YA WATOTO NA VIFAA VYAKE HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI