HALIFA AYAN YUSUF kuiwakilisha Somalia Miss East Africa




Mrembo huyo mwenye urefu wa  futi 5.9 anaitwa HALIFA AYAN YUSUF aliyezaliwa Somalia Hargeisa na ana umri wa miaka 21.
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 mwezi December mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.
Mashindano ya Mwaka huu yanayosubiliwa kwa hamu yanatarajiwa kushuhudiwa na mamilioni ya watu Duniani kupitia kwenye luninga zao na pia kwa njia ya Internet ambapo yatautangaza utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na pia kujenga umoja wa Afrika mashariki na kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa Afrika.
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltdya jijini Dar es salaam

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB