BABYLOVE KALALA AIBUKA MSHINDI REDD'S MISS TALENT 2012
Mgeni Rasmi katika Onyesho la Redd's Miss Talent,Mbunge wa Viti Maalum - Arusha,Mh. Catherine Magige (katikati) akizungumza machache wakati akifungua shoo hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Rino International Agency ambao ni waandaaji wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Giraffe,Dk. Charles Bekon.
Mshiriki namba 30,Waridi Frank akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma za asili.
Mshindi wa Redd's Miss Talent 2012,Babylove Kalala akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma za asili kwa kutimia Nyoka.
Mshiriki namba 11 kutoka Kilimanjaro,Nandi Rafael akionyesha umahiri wake wa kusakata dansi.
Mshiriki namba 29,kutoka Dodoma,Belinda Mbogo nae akisakata Dansi.
Mshiriki namba 3 kutoka Chuo Kikuu Huria,Zuwena Naseeb akionyesha umahiri wake wa kuimba katika onyesho la kumpata mrembo mwenye kipaji lililofanyika katika Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam usiku huu.
Mshiriki namba 13kutoka kanda ya Mashariki,Joyce Baluhi akionyesha uwezo wake wa kusakata dansi.
Mshiriki namba 27 kutoka Ilala,Noela Michael akionyesha kipaji chake cha kuimba.
Mshiriki namba 8 kutoka Kanda ya Ziwa,Happyness Rweyemamu akionyesha kipaji chake cha kuruka sarakasi katika onyesho la kumpata mrembo mwenye kipaji lililofanyika katika Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam usiku huu.
Mshiriki namba 15 kutoka Temeke,Catherine Masumbigana akionyesha kipaji chake cha kupiga Zeze.
Mshiriki namba 7 kutoka Rukwa,Vency Edward akionyesha kipaji alichonacho cha kucheza.