WAZIRI MKUU AONGOZA MAZISHI YA ASKOFU SIMALENGA

PG4A6916Waziri Mkuu, Mizengo pinda akisalimiana na Maaskofu wa kanisa la Anglican nchini wakati alipowasili kwenye kanisa kuu la Anglican la Njombe kuhudhuria mazishi ya Askofu wa Dayosisi  ya South West Tanganyika, , John  Andrew Simalenga Novemba 28, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)PG4A6943Waziri Mkuu, Mizengo Pindaakitoa heshima za mwisho kwa Askofu John Andrew Simalenga katika mazishi ya Askofu huyo wa Dayosisi ya South West Tanganyika ya Kanisa la Anglican lyaliyofanyika Njombe  Novemba 28, 2013.  Kushoto ni Askofu Mkuu wa kanisa la Anglican nchini, Dr. Jacob  Chimeledya.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)PG4A6971Mwili wa Askofu wa Kanisa la Anlican Dayosisi  ya Southa  west, John Andrew Simalenga ukitelemshwa kaburini kwenye mazishi yaliyofanyika wenye kanisa kuu la  Dayosisi hiyo mjini Njombe Novemba 28, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A6981Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge Anne Makinda wakishiki katika Ibada ya mazishi ya Askofu wa Kanisa la Anglican Dayosisi ya South West Tanganyika yaliyofanyika Njombe Novemba 28, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A6996Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka mchanga katika kaburi la Askofu wa Dayosisi  ya  South West Tanganyika ya Kanisa la Anglican, John Andrew Simalenga yaliyofanyika  mjini Njombe Novemba 28, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)PG4A7095Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika ibada ya mazishi ya Askofu wa Kanisa  la Anglican Dayosisi ya South West Tanganyika , John Andrew Simalenga yaliyofanyika Njombe Novemba 28, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A7045Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu wa Dayosisi ya South West Tanganyika , John Andrew Simalenga  katika mazishi yaliyofanyika Njombe Novemba 28, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameongoza mamia ya watu kwenye ibada ya
mazishi ya Askofu wa Saba wa Dayosisi ya South West Tanganyika ya
Kanisa la Anglikana Tanzania Mhashamu Askofu John Andrea Simalengailiyofanyika Njombe mjini.
Akizungumza na mamia ya waumini na waombolezaji waliohudhuria ibada
hiyo ya mazishi leo mchana (Alhamisi, Novemba 28, 2013) Waziri Mkuu
alisema Dayosisi hiyo imepoteza mhimili muhimu lakini akawataka wawe
na umoja na upendo huku wakiendelea kumtumainia Mungu.
“Mhashamu Baba Askofu Simalenga alisimikwa Julai 6, 2008. Ni miaka
mitano tu ya utumishi kwenu na alikuja wakati ambapo Dayosisi hi
ilikuwa imekaa kwa miaka 10 bila ya kuwa na kiongozi. Siku anawekwa
wakfu nilikuwepo na ninakumbuka mlimuomba asaidie kuleta mshikamano,”
alisema Waziri Mkuu.
“Ninawaomba wanadayosisi muwe na upendo na mshikamano mkubwa miongoni
mwenu hadi hapo Mungu atakapotupatia kiongozi mwingine. Tumuombe Mungu
ili kiongozi huyu ajaye apatikane kwa njia ya amani,” alisisitiza.
Alimuomba mke wa marehemu, Bibi Martha pamoja na watoto wa marehemu
waupokee msiba huo kwa mikono miwili na kuahidi kuwaombea faraja kwa
Mwenyezi Mungu.
Waziri Mkuu ambaye alishiriki mazishi hayo kwa niaba ya Serikali,
alitumia fursa hiyo kuwapa pole maaskofu, mapadri, watawa na familia
zikiwa ni salamu maalum kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye alisema
yuko ziarani kwenye mkoa mpya wa Simiyu.
Naye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bibi Anne
Makinda ambaye pia ni mbunge wa Njombe Kusini ilipo Dayosisi hiyo
akitoa salamu za rambirambi alisema wana Njombe wamepungukiwa na nguvu
kwa kuondokewa na Askofu Simalenga.
“Alisaidia kuleta umoja hapa kwetu, tumempoteza mtu muhimu sana katika
harakati za maendeleo ya wilaya yetu na mkoa kwa ujumla. Alisaidia
kuleta umoja na upendo na sisi tuwe na upendo na amani, tuendelee
kumuomba Mungu hadi tutakapoletewa msimamizi mwingine.
Katika mahubiri yake kwenye ibada hiyo, Askofu Mkuu wa Kanisa la
Anglikana Tanzania, Mhashamu Jacob Chimeledya aliwataka waumini wote
wamtazame Mungu na wamtegemee Mungu kwa sababu wanampenda lakini yeye
ameona ni vema ampunzishe mtumishi wake.
“Sote tunajua kuwa katika kipindi chake, Dayosisi hii ilitulia kabisa
je tutaruhusu kuondoka anikwake kuzue tena chokochoko? Msiba huu
usifike mahali ukaanza kututenganisha na kutoa mwanya wa kuanza
kunyoosheana vidole. Tumuombe Mungu atusaidie afute machozi yetu,”
alisema.
Askofu John Andrea Simalenga alizaliwa Novemba 30, 1953 na kufariki
Novemba 24, 2013 baada ya kuugua kwa siku mbili. Novemba 22, 2013
alijisikia vibaya na alipopimwa aliikutwa na malaria, kisukari na
shinikizo la damu. Alilazwa hospitali ya Kibena, Njombe na kuruhusiwa
siku iliyofuata lakini Novemba 24 alizidiwa tena na kuaga dunia.
Ameacha mjane na watoto wanne.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB