Vodacom yazipiga jeki timu za Wawakilishi Zanzibar

Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ali Abdalla Ali (mwenye kofia)akipokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim kwa ajili ya timu ya mpira wa miguu na wa pete za Baraza la wawakilishi. Vodacom imezipatia timu hizo jezi, suti za michezo, viatu na mipira vikiwa na thamani ya Sh 4.5Milioni. Wanaoshuhudia ni Meneja wa timu Nassor Salum Aljazera(kushoto) na Meneja wa Vodacom Zanzibar Mohamed Mansour.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na Vodacom kwa timu za Baraza la Wawakalishi iliyofanyika ofisi za Baraza hilo Mjini Zanzibar. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheri na Naibu Spika wa Zanzibar Ali Abdalla Ali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheri akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na Vodacom kwa timu za Baraza la Wawakalishi iliyofanyika ofisi za Baraza hilo Mjini Zanzibar. Wengine pichani ni Naibu Spika wa Zanzibar Ali Abdalla Ali(katikati) na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Kutoka kushoto: Meneja wa Timu za Baraza la Wawakilishi Nassor Salum Aljazeera, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, Naibu Spika wa Baraza la Wawakalishi Ali Abdala Ali, Meneja wa Vodacom Zanzibar Mohamed Mansour, Makamu mwenyekiti wa Michezo Baraza la Wawawakilishi Mbarouk Mtando na Mweka Hazina wa Baraza Dau Maulid kwa pamoja wakionesha vifaa vya michezo vilivyotolewa na Vodacom kusaidia timu za baraza.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB