Tamko la Chadema Kuhusu Mlipuko wa Bomu katika Mkutano wa Arusha


SAM_2023Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambae pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mh Freeman Mbowe akitoa tamko la chama chake jioni ya leo katika hoteli ya Kibo Palace ya Jijini Arusha kufuatia tukio la kushambuliwa kwa mkutano wa Chadema jana kufunga kampeni za udiwani kwa Kata nne za Arusha Mjini kwa bomu la kutupa kwa mkono, risasi za moto na mabomu ya machozi, tukio lililopelekea vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa. Kushoto kwake ni Bw Samson Mwigamba, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha na kulia kwake ni bw Elifuraha wa redio ya mtandao “ArushaMambo” ya Jijini hapa.
SAM_2026Timu ya waandishi wa habari waliohudhuria kikao hicho cha kutoa tamko la chama. Pichani mwandishi wa Gazeti la Mwananchi, Mussa Juma akiuliza swali kwa mh Mbowe.
SAM_2027
Mwenyekiti wa Chadema Taifa ametoa tamko la chama chake katika hoteli ya Kibo Palace Jijini Arusha. Katika mkutano huo na wanahabari Mbowe amesema na kufafanua yafuatayo:

1. Mh Mbowe amelaani vikali tukio hilo la kikatili kwa raia wasio na hatia...zaidi matumizi ya bomu na risasi za moto

2. Mh amesema shambulio lile ni la kisiasa na lilipangwa kutokea kwa makusudi, sio tukio la bahati mbaya

3. Mh Mbowe amesema hata kama watafanikiwa kumuua yeye Mbowe au Lema bado Chadema itaendelea kuwepo

4. Ameagiza kuwa kuanzia kesho wabunge wote wa Chadema hawatahudhuria vikao vya Bunge na badala yake watashiriki maombolezo Arusha

5. Amesema shambulio la mkutano lilihusisha bomu na risasi za moto zilitumika kuua na kujeruhi viongozi wa chama na wananchi waliofika kusikiliza hotuba mkutanoni hapo.

6. Mbowe amesema huenda ilikuwa yeye afe, ama Lema au viongozi wengine wa Chadema waliokuwa mkutanoni..lakini yeye alisalimika kwa vile alizingwa na watu wengi ambao waliumia ama kufa badala yake.

7. Amehabarisha kuwa Wakala Mkuu wa Chadema uchaguzi wa Makuyuni leo, Joshua Nassary amepigwa vibaya na watu wanaoaminika kukodiwa na CCM na kukimbizwa hospitali ya Selian alikolazwa, nae alikwenda kumjulia hali mchana huu. Mawakala wengine wa Chadema walipigwa na kuamua kukimbia na kuacha vituo vyao kuokoa uhai wao.

8. Mbowe ameongea kwa msisitizo mkubwa kuwa kama CCM na Serikali yake wameshindwa kuheshimu mfumo wa vyama vingi basi waamue sasa kuufuta kabisa

9. Akijibu swali la mwandishi Pamella Mollel aliyehoji Chadema imeanda utaratibu gani katika swala mataibabu ya majeruhi, mh Mbowe amesema kuwa kimsingi jukumu la kugharamia matibabu ya wahanga wa mlipuko na risasi ni la Serikali, lakini kwa sababu za kibinadamu chama chake kitagharamia matibabu ya majeruhi wote.

10. Mh Mbowe hawezi kusema ni nani hasa amehusika na tukio hilo, kwa sasa wanaviachia vyombo vya usalama vitoe taarifa ya uchunguzi wao.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB