MAMA SALMA KIKWETE KWENYE MKUTANO WA SMART PARTNERSHIP 2013

IMG_1282Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Rais wa Sri Lanka Mheshimiwa Mahinda Rajapaksa wakati wa mkutano wa smart partnership dialogue 2013 unaofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere hapa Dar es Salaam kuanzia tarehe 28.6.2013IMG_1425Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akijiandaa kuzungumza na wake wa Marais na Wakuu wa nchi wakati wa mkutano wa smart partnership tarehe 29.6.2013 kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere hapa Dar es Salaam. IMG_1437Baadhi ya wake wa viongozi mbalimbali wanaohudhuria mkutano wa smart partnership wakimsikiliza Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kwenye ukumbi wa Mwalimu Nerere tarehe 29.6.2013.
IMG_1454Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Mke wa Mfalme wa Mswati wa Swaziland, Inkhosikati Lambikiza (kushoto), na Mwakilishi wa Mke wa Rais Joseph Kabila wa DR Congo (kulia) wakimwalika Mke wa Makamu wa Rais wa Zambia Mama Charlotte Scott (hayupo pichani) kujiunga nao katika picha ya pamoja mara baada ya kikao chao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 29.6.2013.IMG_1458Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wake wa Marais na Wakuu wa nchi wanaohudhuria mkutano wa smart partnership unaofanyika hapa Dar es Salaam. Kutoka kushoto no Mama Charlotte Scott, Mke wa Makamu wa Rais wa Zambia akifuatiwa Inkhosikati Lambikiza, Mke wa King Mswati, Mama Salma Kikwete,  akifuatiwa na Mama Siti Hasma, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Malasya Mahathir Mohammed na kulia ni mwakilishi wa Mke wa Rais wa DR Congo.
IMG_1486Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na Mama Siti Hasma mara baada ya kuhudhuria kikao cha wake wa marais na wakuu wa nchi kwenye mkutano wa smart partnership.IMG_1577Mke wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na Inkhosikati Lambikiza wa Swaziland.
IMG_1631Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na Mama Charlotte ScottIMG_1783_1Mama Salma Kikwete na Inkhosikati Lambizana wakijiandaa kwenda katika chakula cha usiku kilichoandaliwa kwenye ukumbi wa mkutano wa Mwalimu Nyerere.
IMG_1833Waziri Mkuu wa Malasya Mheshimiwa Najib Razak akiwa pamoja na Mama Salma Kikwete na Inkhosikati Lambizana wakimwangalia simba dume aliyewekwa nje ya ukumbi wa  jengo la mikutano la Mwalimu Nyerere baada ya viongozi hao kuhudhuria chakula cha usiku tarehe 29.6.2013.
IMG_1842Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na Mfalme Mswati wa Swaziland mara baada ya chakula cha usiku.IMG_1852Rais Jakaya Kikwete akiiagana na Waziri Mkuu wa Malasya Mheshimiwa Najib Razak mara baada ya viongozi hao kupata chakula cha usiku kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere tarehe 29.6.2013.
PICHA NA JOHN  LUKUWI

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB