ZANZIBAR WAFANYA HITMA YA MZEE KARUME LEO
Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wakisoma Hitma Kumuombea Dua Rais wa
kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,katika Ukumbi wa mikutano wa
Ofisi ya CCm Kisiwandui Mjini Zanzibar,ambapo kila ikifika siku kama hii wananchi kwa
ujumla wao hukusanyika kuomba dua kama hii.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,akisalimiana
na wakuu wa Vikosi vya ulinzi alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisdiwandui Mjini
Unguja kuhudhuria katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid
Amani Karume.
Wake wa Viongozi Wakuu wakiwemo na viongozi wa taasisi za Kinamama wakinyanyua
mikono juu kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani
Karume.katika kaburi lake huko CCM Kisiwandui mjini Zanzibar,baada ya kisomo cha Hitma leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein,akisalimiana na wakuu wa Vikosi vya ulinzi alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM
Kisdiwandui Mjini Unguja kuhudhuria katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar
Marehemu Mzee Abeid Amani Karume
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume,(kulia) akiwa na Wake wa
Viongozi mbali mbali katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid
Amani Karume,huko Ukumbi wa CCK Kisiwandui Mjini Zanzibar Leo.
Akina mama wa Kiislamu wa Mjini Magharibi Unguja wakijumuika na Viongozi wengine katika kisomo cha HItmaya Kumuombea Dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar





