AZAM FC YAIPIGA EL NASIR FC YA SUDAN KUSINI MABAO 3-1


8Mchezaji wa timu ya Azam FC Kipre Cheche akiwania mpira katikati ya wachezaji Ladu Manas kulia  na Joseph Odongi  wa timu ya El Nasir FC ya Sudan Kusini katika michuano ya Kombe la Shirikisho uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Timu ya Azam imeibuka na ushindi wa magoli 3-1 ambapo wafungaji wa Mgoli hayo ni Abdi Kassim, Kipre Cheche na John Boko wakati lile la timu ya El Nasir FC limefungwa na mchezaji Fobian Elias, huu ni mwanzo mzuri wa timu ya Azam FC ambapo timu hizo zitarudiana wiki mbili zijazo nchini Sudan Kusini.
9Mchezaji wa timu ya Azam FC Abdi Kassim akipiga mpira wa kichwa na kufunga goli la kwanza mbele ya mchezaji wa timu ya El Nasir FC Simon Amaya.
7Mchezaji Abdi Kasim akishangilia kwa kusujudu mara baada ya kufunga goli la kwanza kwa timu yake huku wachezaji wenzake wakimuangalia.

5Kikosi cha timu ya El Nasir FC ya Sudan Kusini kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
4Kikosi cha timu ya Azam FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
3Wachezaji wakisalimiana
2Wachezaji wakiingia uwanjani tayari kwa mpambano huo jioni hii katika uwanja wa Taifa.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB