WANANCHI WAIPOKEA SEKRETARIETI YA CCM MJINI KIGOMA


1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Ndugu Abdurahman Kinana akishuka kwenye treni mara baada ya kuwasili leo asubuhi kwenye kituo kikuu cha Reli ya kati cha mjini Kigoma a.k.a (Mwisho wa Reli) akiongozana na wajumbe wenzake wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Sekretarieti hiyo iliamua kusafiri kwa  jia ya Treni kutoka jijini Dar es salaam mpaka mkoani Kigoma ambako chama cha Mapinduzi kinaadhimisha miaka yake 36 Februari 3, Mwaka huu, kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.
Lakini Pia Kinana amesema hii ni Kuunga mkono juhudi za Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe na wafanyakazi wa Shirika la Reli (TRL), kwa kuwa na moyo wa kizalendo na kuamua kusimama kidete katika kuhakikisha huduma ya chombo hicho muhimu kwa mikoa ya Magharibi Kinarudi na kuanza kufanya kazi.
12Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdurahman Kinana akizungumza na wananchi waliojitokeza katika mapokezi mara baada ya kuwasili kwa treni na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM mjini Kogoma leo asubuhi.
8Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana na ujumbe wajumbe wenzake wakiwa kwenye kituo kikuu cha reli mkoani Kigoma mara baada ya kupokelewa na wananchi wakitokea jijini Dar es salaam, kulia ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro na Nape Nnauye Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Itikadi na Uenezi.
6Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wakiangalia ngoma mbalimbali zilizoandaliwa na wananchi wa mjini Kigoma kwa ajili ya Mapokezi kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana,Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro na Nape Nnauye Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Itikadi na Uenezi. 
3Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akisalimiana na wananchi wa mjini Kogoma mara baada ya kuwasili kwa treni leo asubuhi mkoani humo.
2Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro na Nape Nnauye Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Itikadi na Uenezi wakishuka kwenye treni mara baada ya kuwasili mkoani Kigoma leo asubuhi.. 
4Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akifurahia jambo wakati Nape Nnauye akishiriki kupiga ngoma na moja ya kikundi kilichokuwa kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Sekretarieti ya CCM baada ya kuwasili mkoani humo ikitoka jijini Dar es salaam.

Popular posts from this blog

TASWIRA: UZINDUZI RASMI WA KAMPENI ZA CHADEMA KWA UDIWANI WA KATA NNE ZA ARUSHA

RAIS KIKWETE ASAIDIA KUENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA WODI YA DHARURA YA WATOTO NA VIFAA VYAKE HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI