Tanzania Red ribbon Fashion Gala 2012 katika picha
Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House na Muandaaji wa Onyesho la Mavazi la Tanzania Red ribbon Fashion Gala,Khadija Mwanamboka (kulia) akikabidhi cheti kwa Mwanamitindo Maarufu nchini,Flaviana Matata ambaye ni Muanzilishi wa taasisi ya kusaidia jamii iliyo kwenye matatizo ya Flaviana Matata Foundation,wakati wa kuadhimisha Miaka Mitano ya Onyesho la Mavazi la Tanzania Red Ribbon Fashion Gala ambalo hufanyika Desemba 1,kila mwaka ikiwa ni kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani,lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam jana.




Mwanamitindo Maarufu nchini,Flaviana Matata (kushoto) ambaye ni Muanzilishi wa taasisi ya kusaidia jamii iliyo kwenye matatizo ya Flaviana Matata Foundation akiongoza mnada wa nguo walizozivaa kwa ajili ya kukusanya hela ya kusaidia wahitaji walio chini ya Taasisi hiyo,ambapo hadi mnada wa vitu mbali mbali unamalizika jumla ya shilingi Milioni 72 ziliweza kukusanywa hiyo jana.Kulia ni Mwanamitindo,Jenuffer Bash.



Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe akiwa na Madam Ritha Paulsen,Maria Sarungi na Mwanamuziki Mkonge nchini,Lady Jay Dee wakati wa Onyesho la Mavazi la Red Ribbon Fashion Gala lililofanyika kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe akienda sambamba na Msanii Linex wakati wakiimba wimbo wa Leka Dutigite ulioimbwa na Wasanii mbali mbali wanaotokea Mkoani Kigoma.
Mh. Zitto Kabwe akiflow na mistari kadhaa ya Wimbo wa Leka Dutigite.
Mh. Zitto Kabwe pamoja na mshabiki wake aliepanda jukwaani kuimba nae wakiaga mara baada ya kumalizika kwa Onyesho hilo.
Mh. Zitto Kabwe akionyesha kitabu ‘SUPER RICH’ kilichoandikwa na Russel Simmons alichonunua kwa thamani ya Shilingi Milioni 4 kama mchango wake kwa kituo cha watoto yatima kinachoongozwa na Mwanamitindo Khadija Mwanamboka cha TMH. Kushoto ni Mwanamitindo wa Kimataifa Mtanzania anayeishi nchini Marekani aliyekuja na bidhaa hizo Flaviana Matata.