MKUTANO WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO TASWA WAFANYIKA BAGAMOYO
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
-
Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwan Kikwete akifungua mkutano mkuu wa chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA unaofanyika kwenye Hoteli ya Kiromo View Bagamoyo mkoani Pwani ambao unajadili mambo mbalimbali ya Maendeleo na changamoto zinazokabili chama hicho.
Waanishi wa habari za michezo ambao ni wanachama kutoka vyombo mbalimbali nchini wanahudhuria mkutano huo ambao ni wa siku moja.
Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Juma Pinto akimkaribisha mgeni rasmi ili kufungua mkutano huo leo asubuhi unaofanyika kwenye hoteli ya Kiromo View Bagamoyo.
Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Amir Mhando akizungumza katika mkutano huo, kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA Maulid Kitenge, Mwenyekiti Juma Pinto, Mgeni rasmi Ridhiwan Kikwete na kushoto ni George John Katibu Msaidizi.
Mtaalam wa SACCOS kutoka Manispaa ya Ilala Bw. Luambano akitoa mada kuweka na kukopa kwa waandishi wa habari wanachama wa TASWA waliohudhuria katika mkutano huo
Kutoka kulia ni waandishi wakongwe Mwina Kaduguda, Mzee Wlly Chiwango na Mzee Salim Said Salim kutoka Zanzibar wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Shafii Dauda, Erasto na Ibrahim Masoud wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Elizaberth Mayemba , Timzo Kalugira na Crala Alphonce wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Kutoka kushoto ni Elius Kambili, Alfred Lucas na Salum Jaba wajumbe wa kamati ya utendaji ya TASWA wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Mgaya Kingoba, Salum Jaba, Richard Mwaikenda na Tulo Chambo wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Wajumbe mbalimbali wakihudhuria mkutano wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA kwenye hoteli ya Kiromo View mjini nje kidogo ya mji wa Bagamoyo mkoani Pwani .
‘Chopa’ iliyotumiwa na Lema ikitua viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro muda mfupi kabla ya kuanza mkutano. Chopa hiyo ilizunguka anga la Jiji la Arusha kwa madoido ya aina yake, hususani katika Kata nne za Themi, Kimandolu, Elerai na Kaloleni, halikadhalika eneo la mkutano, huku ikimwaga vipeperushi vya kunadi kampeni za Chadema na wagombea wake. Blog hii ilishuhudia wananchi wakigombea vipeperushi hivyo vikitua chini. Sehemu ya umati wa wananchi wa Jijini Arusha waliojitokeza jana katika viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro kuhudhuria Mkutano Mkubwa wa Chadema wa Uzinduzi wa Kampeni za kuwania Udiwani kwa Kata nne zilizoachwa wazi na madiwani waliovuliwa uanchama na Chadema zaidi ya miaka miwili iliyopita. Mbunge wa Arusha Mjini na Mjumbe wa kamati Kuu Chadema, Mh Godbless Lema akihutubia umati wa wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo. Mwenyekiti wa Chadema Wilaya, ambae pia ni Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Arusha na Diwani wa Kata ya Levolosi, Mh Ephata Nanyaro...
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa baada ya kuwasili katika hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa katika hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam. Mkurugenzi w...