KAMPUNI YA PRIME TIME PROMOTIONS YATOA MILIONI 105 KUFANIKISHA SHAMRA SHAMRA ZA MKUTANO MKUU WA YANGA


Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi millioni 105 kwa uongozi wa timu ya Yanga kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wao mkuu pamoja na mechi ya kirafiki ya kimataifa katika kukamilisha shamrashamra za kusindikiza mkutano huo wa kwanza wa uwazi wa kihistoria kwa Club ya Yanga. 
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga na Makamu Mwenyekiti wa Club ya Yanga,Clement Sanga wakikabidhiana mikataba yao ya makubaliano ya kikazi.
 Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akitiliana saini ya makubaliano na club ya Yanga kuhusiana na makubaliano ya timu ya Yanga  kusaini mkataba wa maelewano na kampuni ya Primetime Promotions Ltd,ambapo Prime Time Promotions imekubali majukumu ya matayarisho yote ya mkutano wa wanachama wote wa Yanga uliopangwa kufanyika Januari 19 2013.
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akifurahia jambo na baadhi ya Wanahabari mara baada ya kutiliana saini mikataba yao ya kikazi na Club ya Yanga,uliofanyika mapema leo kwenye makao makuu ya ofisi za club hiyo,Jangwani jijiini Dar
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akizungumza machache kuhusiana na makubaliano yao ya kikazi na Club ya Yanga ikiwemo sambamba na makabidhiano ya mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 105 yaliyotolewa na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd.
Pichani kati ni Makamu Mwenyekiti wa Club ya Yanga,Clement Sanga akizungumza mapema leo kwenye makao makuu ya timu hiyo na Waandishi wa habari kuhusiana na timu ya Yanga  kusaini mkataba wa maelewano na kampuni ya Primetime Promotions Lt,ambapo Prime Time Promotions imekubali majukumu ya matayarisho yote ya mkutano wa wanachama wote wa Yanga uliopangwa kufanyika Januari 19 2013.Kushoto ni katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako na kulia ni Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB