RAIS WA ZANZIBAR AENDELEA NA ZIARA YAKE VIETNAM
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa na ujumbe wake wakitoa heshima ya salamu baada ya kuweka shada la mauwa katika kumbusho wa Baba wa Taifa la Vietnam, Ho Chi Minh Mousoleum,akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali,ya wikimoja nchini humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa na ujumbe wake wakiongozwa kwa gwaride maalum wakati alipowasili katika kumbusho wa Baba wa Taifa la Vietnam, Ho Chi Minh Mousoleum,kuweka shada la mauwa,akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali,ya wikimoja.[
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, akiwatambulisha Viongozi aliofuatana nao kwa Makamo wa Rais wa Vietnam Bibi,Nguyen Thi Doan,walipowasili Ikulu ya nchi hiyo kwa mazungumzo,ya kuimarisha uhusiano na Ushirikiano baina ya pande zote, akiwa katika ziara rasmi ya wiki moja nchini humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, akisalimiana na Mawaziri na Viongozi mbali mbali wa Nchini Vietnam ,alipofika ikulu ya nchi hiyo kwa mazungumzo na Makamo wa Rais Vietnam Bibi, Nguyen Thi Doan, akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali nchini humo ya wiki moja.



