SPIKA ANNA MAKINDA ASHIRIKI MKUTANO WA 127 WA IPU, MJINI QUEBEC, CANADA


Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na mratibu wa mahusiano baina yaGlobal Fund na Mabunge Duniani Ndg. Svend Robinson, walipokutana kabla ya kuanza kwa mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Mjini Quebec, Canada
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimtambulisha Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mhe. Dr. Perpetua  Nderakindo Kessy kwa Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex Massinda kabla ya kuanza kwa mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Mjini Quebec, Canada

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifuatilia taarifa mbalimbali na maazimio ya Mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 127 wa IPU Mjin Quebec, Canada. Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex Massinda na Mhe. Hamad Rashid Mohamed
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiongoza ujumbe wa Tanzania kupiga kura kuingiza agenda mojawapo kati ya agenda 5 za dharura zilizowasilishwa kwa udharura katika mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) ili zijadiliwe pia. Tanzania iliungana na nchi za Afrika kupigia kura agenda ya kujadili hali ya usalama katika nchi ya Mali pamoja na agenda iliyowasilishwa na Uingereza kujadili kwa udharura swala la hatma ya Usalama na Misaada wa Kibinadamu Nchini Syria na nchi Jirani. Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex C. Massinda na Mhe. Hamad Rashid Mohamed
Spika wa Bunge akitoka katika ukumbi wa Mikutano mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kwanza katika Mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) mjini Quebec, Canada. Kushoto kwake ni Mhe. David Kafulila anayehudhuria Mkutano huo pia.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisisitiza jambo wakati alipokutana na Spika wa Bunge la Morocco Mhe Karim Ghellab kujadili namna bora ya kuimarisha mahusiano baina ya mabunge ya nchi zao. Tanzania ilipeleka ujumbe wa Wabunge kutoka kamati ya Mambo ya Nje, ulinzi na Usalama kutembelea Bunge la Morocco Aprili mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili

Spika wa Bunge la Morocco Mhe Karim Ghellab akimkabidhi Mhe. Spika zawadi mara baada ya kufanya nae Mazungumzo
Ujumbe kutoka Bunge la Tanzania katika Mkutano wa 127 wa IPU Mhe. Hamad Rashid na Mhe. Suzan Lyimo wakifuatilia kwa makini mada kuhusu “Multilateralism and the role of parliament in parliamentary diplomacy” wakati wa mkutano huo Mjini Quebec, Canada

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB