RAIS KIKWETE NA MKUTANO MKUU WA NANE WA UVCCM MJINI DODOMA LEO


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa UVCCM Bw. Benno Malisa alipowasili ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufungua Mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya hiyo ya vijana wa chama tawala leo Oktoba 23, 2012.
PICHA NA IKULU
Nderemo baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwasili ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufungua Mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya hiyo ya vijana wa chama tawala leo Oktoba 23, 2012.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi maalum Mwakilishi kutoka chama tawala cha  Zimbabwe Chipanga Kudzanai, kutambua mchango wa chama hicho kwa CCM, wakati wa Mkutano Mkuu wa nane wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) leo  Okt 23, mjini Dodoma.
Mjumbe kutoka mkoa wa Mwanza, akipiga kura kuchagua Mwenyekiti, wakati wa Mkutano Mkuu wa UVCCM mjini Dodoma
Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela akitoa utaratibu kabla ya kuanza uchaguzi mkuu wa jumuia hiyo leo mjini Dodoma
Shamra shamra zikihanikiza kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere katika mkutano wa nane wa UVCCM mjini Dodoma
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua mkutano Mkuu wa nane wa Umoja wa Vijana wa CCM mjini Dodoma leo
Wagombea waliokuwa wanawania nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM. Kutoka kushoto, Lulu Abdalla Mshamu ambaye alijitoa wakati akijieleza kwa wajumbe,Khamis Sadifa Juma na Msaraka Rashid Simai ambao ndio waliochuana

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB