MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASIMAMIA UCHAGUZI MKUU WA CCM MKOA WA DAR ES SALAAM



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Mwenyekiti Mpya wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika jana Oktoba 13, 2012 kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba na kutangazwa mshindi katika kinyang’anyiri hicho kwa kupata jumla ya kura 310, huku mpinzani wake J. Guninita akipata kura 214. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi Mkuu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa mchakato huo wa uchaguzi uliofanyika kwenye Ukumbi wa PTA jana Oktoba 13, 2012. Picha na OMR
Baadhi ya mashabiki wa Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na wanachama wa CCM, wakishangilia na kufurahia baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi. Picha na OMR
Baadhi ya wanachama wapiga kura waliohudhuria uchaguzi huo.
Wagombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, kutoka (kushoto) ni Ramadhan Madabida, Chizii na Guninita, kabla ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq, akipiga kura.
Sehemu ya mashabiki na wanachama wa Madabida wakishangilia ushindi wa Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Dar, Badabida.
Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, akisalimiana na baadhi ya wazee wa CCM.

Popular posts from this blog

TASWIRA: UZINDUZI RASMI WA KAMPENI ZA CHADEMA KWA UDIWANI WA KATA NNE ZA ARUSHA

RAIS KIKWETE ASAIDIA KUENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA WODI YA DHARURA YA WATOTO NA VIFAA VYAKE HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI