Wazuiliwa Saudia kwa kukosa 'mahram'


Mecca nchini Saudi Arabia
Serikali ya Nigeria imeteta vikali kuhusu wanawake elfu moja wa nchi hiyo wanaozuiliwa nchini Saudi Arabia.
Wanawake hao ambao wamekuwa wakizuiliwa tangu siku ya Jumapili,walikuwa wanahiji Mecca, lakini wakakamatwa kwakukosa kuandamana na mahram au mwanaume ambaye hawezi kumuoa mwanamke yule mfano babake, kakake au mjomba wake . Mahram pia anaweza kuwa mume wa mwanamke yule.
Mmoja wa wale wanaozuiliwa aliambia BBC kuwa wamenyimwa chakula na kwamba walilazimika kutumia choo kimoja licha ya idadi yao kubwa.
Balozi wa Nigeria nchini Saudi Arabia, Abubakar Shehu Bunu, anashauriana na maafisa katika ubalozi wa Saudia kuhusu hatma ya wanawake hao.
Wadadisi wanasema kuwa wanawake wengi wa Nigeria huingia nchini humo kinyune na sheria ili kufanya kazi ya ukahaba.
BBC swahili

Popular posts from this blog

MH. AMANI ABEID KARUME AFUNGUA SKULI YA DONGE ZANZIBAR