Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lafunika Tabora

Anaitwa Godzilla akiangusha mistari kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mabeste akikamua kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

Mmoja wa wasanii mahiri katika miondoko ya hip hop hapa nchini,Mwana FA akiwaimbisha wakazi wa mji wa Tabora wimbo wake wa Yalaiti, katika viwanja vya Ally Hassan Mwinyi.

Nikki wa Pili akishusha mistari yake mbele ya wakazi wa mji wa Tabota.

Msanii wa muziki na pia ni muigizaji wa filamu,anaitwa Shilole akitumbuiza kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,mjini Tabora.

Rich Mavoko akiliongoza skwadi lake kusakata kiduku
